AMINI AFUNGUKA NA KUSEMA HATAKI MALUMBANO NA LINAH

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya, Amini Mwinyimkuu amesema hataki malumbano na mpenziwe wa zamani Linah Sanga na badala yake ameamu kunyamaza kimya.

Amini alisema hayo kufuatia ushauri kutoka kwa Linah akimtaka badilike ili asipotee kwenyue muziki huo, kauli ambayo anaona ni mashabulizi dhidi yake.

Amini alikaririwa akisema kuwa Linah kwa sasa si yule wa zamani katika uimbaji anakosa uyeye aliokuwa nao mwanzo enzi zile Amini alipokuwa akimwandikia nyimbo, kwamba nyimbo anazozipata sasa hivi sio za kuimbwa na kimwana huyo.


Hata hivyo Linah amemtaka Amini asiseme kuwa yeye Linah amepotea kwani hata yeye mwenyewe hajulikani alipo na kumtaka abadilike ili kukabiliana na ushindani iliopo kwenye muziki.

No comments