ANDY WALKER APONDA MOURINHO KUWAZOGOA MABEKI CHRIS SMALLING, LUKE SHAW

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Celtic, Andy Walker amesema anadhani kauli ya kocha Jose Mourinho kabla na baada ya mechi dhidi ya Swansea City kuhusiana na mabeki Chris Smalling na Luke Shaw ni sawa na kuwafungulia mlango wa kuondoka Manchester United.

Mabeki hao hawakuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha kwanza kwenye mechi ya ushindi ya mabao 3-1 dhidi ya Swansea City.

Kocha Mourinho aliiambia televisheni ya MUTV kuwa wachezaji hao walielielezwa kuwa hawatacheza mechi hiyo kwa vile hawakuwa fiti.

Walker anadhani kuwa kauli ya Mourinho baada ya mechi dhidi ya wachezaji hao haikuwa sahihi.

“Angalia wachezaji aliowahi kufanya nao kazi kama John Terry [Frank] Lampard, Seargio Ramos na Pepe unaweza kuwatolea kauli kama hiyo,” alisema.

“Nadhani hakuwa sahihi kusema hana imani na Luke Shaw au Chris Smalling. Inapokuja mechi kubwa kisha unawaambia hawana nafasi inamaana ni sawa na kuwaambia waondoke.”


“Ni kama vile kuna aina fulani ya wachezaji ndio wanaoonekana na pengine Smalling na Shaw sio chaguo lake.”

No comments