ARSENAL YAITUNGUA BOURNEMOUTH 3-1 NA KUFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA


ARSENAL imeichapa Bournemouth 3-1 katika mchezo wa Premier Legue na kuzidi kuzipumulia kwa karibu timu za Manchester City, Liverpool na Chelsea zilizoko kileleni mwa msimamo wa ligi.

Alexis Sanchez aliifungia Arsenal mara mbili dakika ya 17 na 90 wakati Theo Walcott alifunga dakika ya 53 huku bao pekee la Bournemouth likifungwa na Callum Wilson kunako dakika ya 23.No comments