AUNTY EZEKIEL: SIWEZI KUBWETEKA NA KUTEGEMEA FILAMU PEKEE

MWIGIZAJI wa filamu Aunt Ezekiel amesema kuwa hawezi kubweteka kwa kutegemea fani hiyo tu bali anafanya biashara nyingine inayomsaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Mtu kuwa na shughuli ya ziada ni jambo la kawaida katika maisha ndiyo maana mbali na kuigiza nimekuwa nikifanya shughuli nyingine za kuniongezea kipato,” alisema Aunt.

Alisema si kwamba anafanya biashara kama walivyoamua kufanya baadhi ya wasanii baada ya Bongomuvi kukumbwa na changamoto bali amekuwa ni mjasiriamali wa siku nyingi.


Alisema kuwa anamuomba Mungu aendelee kunyoosha mkono juu yake kwa kufanikisha malengo aliojiwekea kwa ajili ya maisha ya familia akiwamo mtoto wake Cookie na mpenzi Moze Iyobo.

No comments