BABY JAY AFICHA MAJINA YA NYIMBO ZAKE AKIHOFIA KUIBIWA

BABY Jay anahofia kuibiwa ubunifu wake katika muziki hivyo hayuko tayari kutaja majina ya nyimbo zake mpya alizokamilisha hadi hapo atakapozitambulisha rasmi.

Alisema kuwa kwa sasa kuna wasanii wanaokaa kuvizia wenzao wataje majina ya nyimbo na kisha wayachukue na kugeuza yao hali ambayo inasababisha nyimbo nyingi kufanana majina.

“Ukufuatilia kwenye muziki wa Kizazi Kipya utagundua kwamba kuna wasanii ambao nyimbo zao zinafanana majina, mimi sitaki iwe hivyo kwa sababu ninajua hasara yake,” alisema.


Alisema kuwa anajiandaa kutambulisha nyimbo zake  mwezi ujao na ndipo majina yake yatajulikana kwa vile anaweza kuyataja sasa na kukuta yameshachukuliwa na wengine.

No comments