BAO LA DOUGLAS COSTA LAIFANYA BAYERN MUNICH KUFIKISHA BAO LA 400 LIGI YA MABINGWA

BAO lililofungwa usiku wa kuamkia juzi na staa Douglas Costa limeifanya Bayern Munich kufikisha mabao 400 katika historia yake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na ndilo lililowafanya mabingwa hao wa Ujerumani kuwa mbele dhidi ya Rostov kabla ya mambo kuwaenea kombo.

Staa huyo raia wa Brazil alifunga bao hilo dakika ya 36 ya mchezo huo ambao ulipigwa nchini Russia baada ya shuti lililochongwa na Renato Sanches kutoka eneo gumu kutemwa na mlinda mlango Soslan Dzhanaev.


Kwa kufikisha idadi hiyo, Bayern Munich kwa sasa inashika nafasi ya tatu ya timu fungaji bora za muda wote katika michuano hiyo nyuma ya Real Madrid yenye mabao 481 na Barcelona yenye 447.

No comments