BARCELONA, MAN CITY WAMWANIA MESUT OZIL... uongozi wa Arsenal wanahaha kuwaongezea mkataba mrefu

TIMU ya Barcelona inaongeza kasi ya kuipata saini ya nyota wa washika mitutu wa jiji laLondoni, Arsenal, Mesut Ozil.

Pamoja na Barcelona pia matajiri wa jiji la Manchester City nao wanaoingia katika mbio za kumwania Bellerin katika usajili wa mwezi Januari mwakani.

Bellerin ambaye ni raia wa Hispania amebakiza kandaraasi ya miaka mitatu ya kubakia Emirates huku akiwa hajaanza mazungumzo mapya na uongozi wa washika mitutu wa jiji la London.

Nyota huyo aliyejiunga na Arsenal mwaka 2011 akitokea Barcelona amekuwa katika kiwango cha juu kwa sasa hali ambayo kocha Arsene Wenger ameutaka uongozi kupigana kwa ajili ya kumbakiza.

Hata hivyo Bellerin wenyewe ameonyesha dhamira za dhati za kutaka kurejea Barcelona ingawa pia kuna tetesi kuwa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameonyesha azma ya kumwania.

City wameanza mazungumzo ya chinichini ya kumwania nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 huku wakiamini kuwa atakuwa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi inayoongozwa na Pablo zabaleta na Bacary Sagna.

Hata hivyo Arsenal wanaonyesha hawapo tayari kumwachia Bellerin na tayari wameanza harakati za kuketi naye mezani kwa ajili ya kumshawishi aongeze kandarasi mpya.

Taarifa za ndani za “The Genners” zinasema kuwa wanahitaji kumuongezea kandarasi inayoweza kuishia mwishoni msimu wa mwaka 2022 juu nya mkataba wake wa sasa.


Pamoja na Bellerin pia uongozi wa Arsenal wanahaha kuwaongezea mkataba mrefu wanandinga wawili ambao ni Mesuti Ozil na Alexis Sanchez ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu mwaka 2018.

No comments