MWIMBAJI wa R&B, Belle 9 amesema bado anatafakari kama ajitose kwenye muziki wa Singeli ama aache kwa madai kwamba muziki huo ni sawa na Big G ambayo inatafunwa na kuisha utamu mara moja.

Belle 9 alisema kuwa ni vyema kujipa muda wa kutosha wa kutafakari badala ya kukurupuka kumbe hauna uhai mrefu kama ilivyo mitindo mingine ya muziki.

“Sio kwamba ninaidharau Singeli bali wasiwasi wangu ni kuwa muziki huo sio wa kudumu, unaweza ukatoweka ghafla hivyo siwezi kuufanya hadi hapo nitakapojiridhisha,” alisema.


“Naifagilia Singeli kwa sababu ni muziki unaowakilisha baadhi ya makabila hapa nchini lakini narudia kwamba sijafikiri kutoa wimbo katika mtindo wa Singeli.”
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac