BOSI BAYERN MUNICH AMSHAURI BASTIAN SCHWEINSEIGER AONDOKE MAN UNITED

MKURUGENZI mtendaji wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amemtaka mchezaji wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger kuondoka katika klabu hiyo pamoja na kuwa amerejeshwa katika kikosi cha kwanza kwa ajili ya mazoezi siku ya Jumatatu.

Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akicheza na kufanya mazoezi na kikosi cha vijana wa klabu hiyo tangu Mourinho achukue timu baada ya Louis Van Gaal kutimuloiwa mapema baada ya msimu kumalizika.

Bastian, mchezaji na kungo wa zamani wa Bayern alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza siku ya Jumatatu, ingawa kumekuwa na taarifa pia kutoka chombo cha habari cha Ujerumani maarufu kama “Sport 1” kilichosema kuwa amekuwa akiwekwa kwenye miundo tofauti ya mazoezi kumwandaa kurejea kikamilifu katika kikosi cha kwanza.

Hata hivyo Rummenigge ambaye alitoka hadharani mapema msimu huu kumpinga Mourinho mwezi Agosti, aliliambia Bild: “Ninachomshauri na ninachofikiri kuwa ni vyema akatafuta suluhisho la mapema la wapi atacheza pale ambapo dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Junuari.”

Rummenigge pia alihoji namna ambavyo Mourinho amelisimamia hili suala akisema: “Ni ngumu kuendana na mabadiliko ya nyakati, lakini hilo halina mashiko, unachotakiwa kufanya ni kuwa na mbinu sahihi za kiutendaji.”

Schweinsteiger ambaye alisema hatakuwa tayari kuchezea klabu nyingine yoyote Ulaya kama ataondoka United, aliapa kuwa tayari kucheza pindi atakapohitajika na baada ya kutokea kwenye mazoezi baadae alienda kwenye Twitter na kusema: “Nimejisikia vyema leo! Timu ipo vyema, matokeo yatafuata!”

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2014, Schweinsteiger alirudi katika mazoezi na kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Kiungo huyo amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 23 tangu Jose Mourinho alipoteuliwa kuwa kocha msimu huu.


Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwa mara ya mwisho aliichezea Manchester United mwezi Machi wakati Louis Van Gaal alipokuwa kocha wa mashetani hao wekundu, alisema mwezi Agosti kuwa hana tatizo binafsi na Mourinho na Man United itakuwa klabu yake ya mwisho kucheza barani Ulaya.

No comments