CHUCHU HANS AIPIGIA DEBE KAMPUNI YAO NA RAY KIGOSI

MWIGIZAJI Chuchu Hans amesema kuwa mkakati mkubwa wa kampuni ya filamu ya “Chura” ni kuibua na kukuza vipaji vya wasanii wanaochipukia ili wawe nyota wa baadaye.

“Chura sio kampuni mpya ingawa haina muda mrefu, tumeianzisha mimi na mpenzi wangu Ray kwa lengo la kusimamia filamu, lakini pia tukilenga kukuza vipaji vya wasanii wanaochipukia,” alisema.

Alisema kuwa baada ya miezi michache ijayo kile kinachofanywa na Chura kitaanza kuonekana ili kuziba midomo ya wale ambao wamekuwa hawaamini kwamba kuna kampuni hii kwani wapo ambao wamekuwa hiyo.


“Tunasemwa sana hata kwenye mahusiano yetu na pia kuanzishwa kwa kampuni hii wapo ambao wamekuwa wakitusema lakini kadri wanavyotusema ni kama wanatufungulia njia ya mafanikio,” alisema.

No comments