CHELSEA, MANCHESTER UNITED VITANI KUMWANIA MLINZI ANTONIO RUDIGER WA ROMA

MATAJIRI wa Darajani chini ya kocha Antonio Conte wameingia katika vita vya utajiri na Manchester United.

Klabu hizo zote zap rimier zinamwania mlinzi wa labu ya Roma ya Italia, Antonio Rudiger.

Chelsea tayari wameweka mezani dau la pauni mil 35 kwa ajili ya kupata saini ya beki huyo ambaye kwa sasa yuko katika kiwango kizuri.

Kocha Antonio Conte anamtambua vizuri Rudiger tangu alipokuwa akifundisha ndani ya Ligi ya serie A.

Mlinzi huyo raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, anatakiwa pia na klabu za nchini ispania, zikiwemo Atletico Madrid na Real Madrid.

Rudiger ambaye ni mlinzi tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani aliumia kifundo cha mguu, hata hivyo Chelsea wamesema watamvumilia mpaka aone na kuendelea na mazungumzo ya kumsajili katika dirisha la Januari.

Kocha Conte amethibitisha kumwania Rudiger baada ya kutokamilika kwa mpango wa kuwania saini ya Lenaldo Bonucci na Kalidou Koulibaly ambao walikuwa wakiwindwa katika usajili wa majira ya kiangazi.


Pamoja na Rudiger, pia kocha Conte amewaweka katika rada za usajili wa mwezi Januari Michael Keane na Ben Gibson.

No comments