CHIPUKIZI PURAB KOHLI WA BOLLYWOOD AINADI FILAMU YAKE MPYA YA "ROCK ON 2"

MWIGIZAJI anayechipukia na kutikisa medani ya Bollywood, Purab Kohli amewataka mashabiki wake wakae tayari kutokana na ujio wa filamu yake mpya ya “Rock On 2”.

Kohli aliuambia mtandao wa The Times of India kwamba licha ya matatizo aliyoyapitia lakini kwa sasa ameimarika na anatarajia kuitangaza vyema kazi yake.

“Naamini nitafanya vizuri zaidi na ndio maana nimetangaza kwamba huu ndio ujio wangu mpya, sitegemei kurudi nyuma kamwe,” alisema.

No comments