CRISTIANO RONALDO AFUNGUKA UPINZANI WAKE NA LIONAL MESSI

STRAIKA Cristiano Ronaldo amefunguka kuhusu upinzani wake na staa mwenzie, Lionel Messi akisema kwamba hawana urafiki hata siku moja ila kilichopo ni kwa kila mmoja kumheshimu mwenzake.

Katika kipindi cha miaka minane iliyoipita, nyota hao wa Real Madrid na Barcelona wamekuwa wakipokezana tuzo ya mchezaji bora wa Dunia “Ballon d’Or” na inasemekana kuwa ndio wachezaji bora kwa sasa katika tasnia hiyo ya soka.

Kutokana na hali hiyo kumrekuwa kukizuka mjadala kuhusu ni yupi bora kati ya wawili hao, lakini hivi karibuni Ronaldo akasema kuwa hakuna vita kati yao.

“Kuna heshima kubwa kati yangu na Messi,” staa huyo mwenye umri wa miaka 31 aliliambia jarida la Coach Magazine.


“Vyombo vya habari vimekuwa vikikuza mambo kwamba tuna uhasama mkubwa, lakini sio kweli licha ya kuwa hatuna urafiki mkubwa lakini kuna kuheshimiana pande zote mbili,” aliongeza staa huyo. 

No comments