CRISTIANO RONALDO, LIONEL MESSI WAINGIA VITA YA MKWANJA

ACHANA na vita ya kuwania kupiga “Hat Trick” nyingi, sahau hekaheka ya kusaka rekodi ya kupachika mabao mengi La Liga au Ligi ya Mabingwa Ulaya mahasimu Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona wana vita nyingine nje ya uwanja.

Vita yao nje ya dimba ni mkwanja wanaolipwa mastaa hao kila mmoja anakunja pauni 365, 000 kwa wiki (sh. mil 970).
Pamoja na Galeth Bale kusaini mkataba mrefu wa miaka sita Real Madrid, bado hajaweza hajaweza kuwafikia nyota hao kwa kipato.

Mwanzoni mwa wiki hii Bale aliongeza mkataba utakaomfanya kubaki hapo hadi mwaka 2022 na kulipwa pauni 346,000 kwa wiki (sh. mil 919).

Hata hivyo mkataba mpya wa Bale umemleta nafasi ya tatu miongoni mwa wanasoka wenye kipato kikubwa nyuma ya Ronaldo na Messi.


Katika mkataba wake mpya wa Bale atavuna pauni mil 108 (sh. bil 287).

No comments