DAVID MOYES AADHIBIWA MECHI DHIDI YA SOUTHAMPTON

KOCHA wa Sunderland, David Moyes alifukuzwa kutoka eneo wanamokaa wakufunzi na kulazimishwa kukaa maeneo ya mashabiki wakati wa mechi dhidi ya Southampton Kombe la EFL usiku wa Jumatano iliyopita.

Sundeland walilazwa 1-0 na Saints na kuondolewa kutoka kwenye michuano hiyo.

Sofiane Doufal aliyenunuliwa pauni mil 16, alifunga dakika ya 66, ikiwa mechi tatu mtawalia Black Cats kushindwa.

Sunderland wameshinda mechi mbili pekee chini ya meneja huyo wa zamani wa Manchester United.

Moyes aliadhibiwa dakika za mwishomwisho za mechi hiyo baada ya kulalamika kwamba klabu yake ilifaa kupewa penati.


Ombi lake likakataliwa na mwamuzi Chris Kavanagh.

No comments