DIEGO SIMEONE AMPIGIA SALUTI KEVIN GAMEIRO

KOCHA Diego Simeone amempigia salti straika wake Kevin Gameiro kwa kuizamisha PSV katika mchezo ambao atletico Madrid waliondoka na ushindi wa mabao 2-0 na kuwafanya wakae kileleni mwa msimamo w kundi D katika michuano ya ligi ya mabingwa uliopingwa usiku nwa kuamkia Alhamisi iliyopita mjini Madrid.

Katika mchezo huo Gameiro ndiye aliyeipatia timu yake bao la kuongoza muda mfupi baada ya timu hizo kutoka mapumziko na kisha Antoine Grezmann akiongeza la pili zikiwa zimebaki dakika 24 kabla ya mchezo kumalizika lakini alikuwa ni nyota huyo wa zamani wa Sevilla ambaye aliukonga zaidi moyo wa Simeone.

"Kwa ujumla kilikuwa ni kipindi cha pili ambapo alionekana kutulia na wakati huo tulikuwa tumekaliwa kooni lakini Gameiro alitutuliza kwa kutoa pasi ambazo ziliturejesha katik mchezo,” Simeone aliwaambia waandishi wa habari.


“Gameiro pia alicheza vizuri kipindi cha kwanza na alipata nafasi kadhaa. Bao lake lilionesha ubora kasi, nguvu na umaliziaji wake ulikuwa ni wahali ya juu,” aliongeza kocha huyo.

No comments