DK. CHENI AGOMA KUENDELEA KUTOA FILAMU… kisa? Wizi wa kazi za wasanii na serikali kuonekana kufumbia macho

WIZI wa kazi za wasanii ambao umekuwa ukiripotiwa kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini umesababisha mkongwe wa Bongoimuvi, Dk. Cheni kufanya maamuzi magumu.

Nyota huyo amesema kwa sasa hawezi kucheza tena filamu hadi hapo serikali itakapohakikisha kuwa filamu zinalindwa dhidi ya wizi wa kazi za wasaniii.

Cheni aliiambia eNews ya EATV kuwa usalama wa kazi za wasanii ndio tatizo kwenye tasnia ya filamu nchini, hali inayosababisha wasanii kukata tamaa.

“Siwezi kutoa tena filamu hadi serikali itakapohakikisha kazi zetu zipo salama, ukitoa filamu leo siku moja ya pili, ya tatu unazikuta chini barabarani zinauzwa feki,” alisema Cheni.

No comments