DOGO JANJA AWATAKA WEUSI KUZUNGUMZA NA TIPTOP KAMA KWELI WANAMTAKA

KUFUATIA tetesi za kutakiwa na kundi la Weusi, mkali wa wimbo “Kidebe” Abdulazizi Abubakar “Dogo Janja” ameutaka uongozi wa kundi hilo kukutana na uongozi wa kundi la Tiptop wazungumze kuhusu suala hilo.

“Mimi sijui lolote kuhusu taarifa hizo lakini kama Weusi wananitaka wakae chinbi waongee na uongozi wangu kwasababu mimi niko chini ya TipTop, sina mamlaka ya kufanya lolote, ila kama wananitaka wazungumze maana mimi na weusi ni marafiki,” alisema Dogo Janja.


Msanii huyo yuko chini ya TipTop yenye maskani yake Manzese na kwa sasa kundi hilo lipo kimya tangu waachie wi,mbo wao wa pamoja “Ridhiki”.

No comments