DROGBA AMKINGIA KIFUA SWAHIBA WAKE MOURINHO... asema hajaishiwa, aomba apewe muda kuisuka United

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesesitriza kuwa Jose Mourinho hajaisha na kuomba apewe muda kuisuka Manchester United.

Drogba ni rafiki wa kocjha huyo na kwa miaka mingi walikuwa pamoja Chelsea.

Mourinho alimsajili Drogba na kumtengeneza kuwa miongoni mwa wanaasoka nyota duniani kwa kuipa Chelsea mataji.

Manchester United imekuwa ikisuasua kwenye Ligi Kuu England licha ya kumuajili Morinho.

Mourinho alianza kwa kishindo kwenye kikosi cha timu hiyo kwa kuisaidia kushinda Ngao ya Hisani.

Hata hvyo kikosi hicho kimeyumba kwenywe Ligi Kuu England licha ya kusheheni nyota wa bei mbaya.

Mourinho alitumia fedha nyingi kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wanne.

Manchester United ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri msimu huu lakini hali imekuwa kinyume chake.

Drogba anaamini Manchester United itafanya vizuri kama Mourinho atapewa muda wa kuisuka.

“Mourinho hajaisha, nadhani anachohitaji ni kupewa muda ili kutengeneza timu,” aliongeza Drogba.

Drogba aliionya Manchester United haitashinda ubingwa bali Mourinho anatakiwa apewe muda wa kutengeneza timu ushindi.

Manchester inashika nafasi ya sita katika Ligi Kuu England ikiwana pointi 18.


Ina mtihani mgumu wikiendi ijayo wa kukabiliana na Arsenal kwenye Ligi Kuu ya England.

No comments