DULLY SYKES ASEMA SIO LAZIMA KILA MSANII AJUE KUTUNGA NYIMBO

DULLY Sykes amewataka wasanii wenzake wa muziki wa Kizazi Kipya kuacha kulazimisha kutunga nyimbo huku wakiwa hawana uwezo huo na badala yake wakubali kutungiwa ili waweze kutoa kazi zenye ubora.

“Binafsi ninaamini kwamba msanii mzuri ni yule anayekubali kuandikiwa nyimbo na sio kulazimisha wakati hana uwezo kwani hata mimi wakati mwingine ni mmoja wa watu wanaokubali kuandikiwa nyimbo,” alisema.

Alisema kuwa hata wimbo wake mpya wa “Inde” hakuanda peke yake bali msanii wa WCB, Rayvanny alishiriki kwenye kuandika mashairi na kwamba huo ndio utaratibu mzuri wa kuandaa nyimbo.


“Kwenye muziki huwa niko wazi kwasababu ninajua kwamba mtu kuwa msanii sio lazima ajue kutunga nyimbo, ingawa mimi ninajua kutunga, lakini wapo baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakilazimisha vitu ambavyo hawaviwezi,” alisema.

No comments