ERIC CANTONA AMTAKA JOSE MOURINHO KUZIDI KUKOMA ILI ASIUMBUKE

KOCHA mpya wa Manchester United, Jose Mourinho ameshinda mechi nane tu katika 16 hadi sasa.

Rekodi hiyo ni mbaya kuliko hata zilizoachwa na watangulizi wake Old Trafford, David Moyes na Louis Van Gaal.

Na lewo rekodi yake inaweza kuharibika zaidi, labda washinde mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Swansea watakapokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Lakini mkongwe wa Man United, Eric Cantona hataki kumshusha uwezo kocha huyo Mreno badala yake anamtaka kukomaa.

Cantona anaamini kuwa kinachomkuta kocha huyo mpenda mazungumzo, kwa sasa ni mapito magumu, lakini anaamini ni suala la muda tu.

“Nafahamu njia ngumu anayopita kwa sasa,” alisema Cantona.

“The Special One (Mourinho), Msweden (Zlatan Ibrahimovic), mchezai wa bei mbaya anayependa kutengeneza nywele (Paul Pogba) na Wayne Rooney, hawa wote hawajaonyesha makalai yao hadi sasa.

“Lakini kwanini wasipewe muda? Soka sio sawa na soimo la sayansi.”


“Komaa mwanangu Mourinho bila hivyo mambo yatakuwa magumu kwako. Kufundisha Manchester United sio sawa na kufundisha Sunderland.”

No comments