FEZA KESSY: SINA UTANI KWENYE KAZI NDIO MAANA NAENDELEA KUPATA MAFANIKIO

FEZA Kessy amesema kuwa hana utani kwenye kazi ndiyo maana ameendelea kupata mafanikio makubwa kwenye muziki wa Kizazi Kipya na hata kupata ajira kirahisi kwa sababu ya kujituma.

Alisema kuwa hana muda mrefu kwenye muziki lakini ameshavuka mipaka ya Tanzania kwa sababu anajituma inavotakiwa na kuwafanya mashabiki wamkubali.

“Wapo watu ambao wamekuwa wakidhani kwamba nimependelewa ama kuna mtu ananishika mkono kupata ajira au katika shughuli zangu za muziki lakini ukweli ni kwamba nina sifa zinazoendana na pia ninajituma kikamilifu,” alisema Feza


Alisema kuwa ameingia kwenye tuzo za EATV kwa wimbo wake wa “Sanuka” kwa sababu anajituma na siyo kubweteka na kungojea kubebwa.

No comments