GABO ZIGAMBA AZIMIMINIA SIFA TUZO ZA EATV

NYOTA wa Bongo Movies Gabo Zigamba amechangamkia tuzo mpya zilizoanzishwa na EATV ziitwazo EATV Awards na kusema kuwa zitaleta ushindani na kutambua mchango wa msanii wa filamu nchini.

Msanii huyo alisema kuwa yeye binafsi ameshiriki kwenye tuzo hizo na ana imani ndiye mtu wa kwanza kupeleka fomu baada ya kusikia tu kuhusu kuwapo kwa tuzo hizo.

Gabo alisema hayo alipokuwa akizungumza na EATV na kufafanua kuwa tuzo hizo ni changamoto kubwa kwa wasanii kwa vile zitatengeneza ushindani hasa kwa kuzingatia kwamba upande wa filamu kwa muda mrefu kumekuwa hakuna kitu cha kuwafariji.


Alisema kuwa katika tasnia ya filamu hakuna tuzo za aina hiyo hivyo tuzo iliyoletwa na East Africa Televisheni anichukulia kama kitu ambacho kitatengeneza ushindani.

No comments