GABO ZIGAMBA AZIUPIGIA UPATU TUZO ZA EATV... awataka wasanii wenzake kuwa na tamaduni wa kuchangamkia vitu vya kwao

MSANII wa Bongomuvi Salim Ahmed "Gabo" amewataka wasanii wenzake kuwa na utamaduni wa kuchangamkia vitu vya kwao badala ya kukimbilia nje ya nchi.

Alisema kuwa alitarajia wasanii nyota watajitokeza kwenye king’ang’aniro cha tuzo za EATV zinazotarajiwa kutolewa Desemba  10, mwaka huu zikishirikisha pia wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya.


“Watu wameshindwa kuamka na kuona cha kwetu na kukichangamkia sijui kwanini kumekuwa na ugumu labda ni ugeni wa tuzo hizo ndiyo umewafanya wasanii nyota kutojitokeza kwa wingi,” alisema.

No comments