GARETH BALE ATETEA KUONGEZA MKATABA MPYA REAL MADRID

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Gareth Bale amesema kwamba anajisikia kama yuko nyumbani akiwa katika kikosi hicho ndio maana ameongeza mkataba wa kuendelea kubaki katika timu hiyo.

Amesema kwamba pamoja na ukweli kuwa kuna timu zilikuwa zinamtaka, lakini ameona ni jambo jema kama atabaki katika timu yake hiyo ambayo amesema ameizoea na inampa heshima kubwa.

Bale ambaye uhamisho wake ulivunja rekodi ya dunia 2013 alipojiunga na Real Madrid, sasa amepata mkataba mpya ambao utamfanya kuwa mali ya klabu hiyo hadi mwaka 2022.

Bale, mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013 akiwa katika kiwango cha juu kabisa.

Tayari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya Ulaya mara mbili huku akifunga magoli 62 katika michezo 135.

Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia waisaini mkataba mpya mwezi huu na kuondoa kabisa uvumi kwamba walikuwa wanahamia kwenye timu nyingine.

Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa euro 600,000 kwa wiki, huku baada ya makato ya kodi ikiwa euro 350,000.

Hata hivyo amesema kwamba anataka kubaki katika timu hiyo kwasababu anajua ni kubwa na yenye heshima kubwa pia.


“Kama unataka kuondoka Real Madrid unatakiwa pia utafakari sana kwamba unakwenda wapi kwenye heshima na thamani zaidi ya hapa, ukikosa majibu maana yake akili yako inatakiwa kuendelea kukubali ukweli kwamba Real Madrid ni timu kubwa na yenye heshima kubwa pia,” amesema.

No comments