GARY NEVILLE AUSHUTUMU UONGOZI WA CHAMA CHA SOKA ENGLAND KWA “UNDUMILAKUWILI”

KOCHA msaidizi wa zamani wa England, Gary Neville ameushutumu uongozi wa chama cha soka nchini England kwa “undumilakuwili” kwa kushindwa kuwaadhibu mastaa Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wanatuhumiwa kuibuka shoo ya wanawake wanaocheza wakiwa utupu kwenye klabu ya usiku katika mji wa Bournemouth.

Nyota hao wa Liverpool walipewa onyo baada ya kubainika nao waliibuka kwenye klabu ya usiku wakati wakiwa kwenye kambi ya England.

Wayne Rooney ambaye ni nahodha wa England alilazimishwa kuomba radhi mbele ya wenzake baada ya kulewa chakari na kuvamia harusi wakati wa kambi ya timu hiyo ya kujiandaa na mechi za michuano ya awali ya Kombe la Dunia na ile ya kirafiki dhidi ya Hispania.


“Ninashindwa kuelewa haya mambo. Rooney alilazimishwa kuomba radhi mbele ya wenzake lakini wengine waliokuwa na makosa kama hayo wakaachwa,” aliandika Neville kwenye mtandao wa Twitter.

No comments