GUARDIOLA AAMINI TAJI LA LIGI KUU NI LA MANCHESTER CITY MSIMU HUU

LICHA ya kikosi chake kukosa ushindi katika michezo sita mfululizo, kocha wa Manchester City Pep Guardiola anaamini kikosi chake kina nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mhispania huyo kucheza mechi sita bila kuibuka na ushindi.

Hata hivyo Guardiola hajakatishwa tama na majanga hayo na badala yake amesema ana uhakika wa kuchukua mataji msimu huu.


“Ndio. Ni mechi sita bila ushindi, hali si nzuri. Lakini tumeondoshwa kwenye moja ya mashindano (Kombe la Ligi), lakini badoi tuna mataji matatu,” alisema Guardiola.

No comments