GUARDIOLA ASUBIRI KUOMBWA MSAMAHA NA YAYA TOURE

KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola anamwitaji kiungo wa kati, Yaya Toure, lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na wakala wa kiungo huyo.

Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 33, amecheza mara moja msimu huu katika Kombe la Klabu Bingwa.

Baadae aliachwa nje katika kinyang’anyiro hicho. Dimitri Seluk alidai kuwa Toure amefedheheshwa na uamuzi huo.

Alipoulizwa iwapo Toure angecheza katika Kombe la Ligi katika uwanja wa Old Trafford, Guardiola alisema: “Unajua hali ilivyo?”

Raia huyo wa Uhispania alisema mnamo mwezi Septemba kuwa Seluk lazima aombe msamaha iwapo Toure anahitaji kucheza kwenye kikosi cha kwanza lakini ajenti huyo aliiambia BBC Sport wakati huo kwamba: “Ni nini ninachofa kukiombea msamaha? Anafaa kuongea na Yaya anayemfanyia kazi yake.”


Na huku kukiwa hakuna msamaha uliotolewa, hakuna mapatano kati ya mkufunzi huyo na mchezaji wake.

No comments