HARMONISE ASEMA HANA MPANGO WA KUANDAA ALBAMU KWA SASA... asema ataendelea kutoa singo mojamoja na kuingiza sokoni

MSANII anayekuja kwa kasi zaidi katika muziki wa Kizazi Kipya, "Harmonize" amesema kuwa hana mpango wa kuandaa albmu na badala yake ataendelea kutoa singo na kuingiza sokoni.

Alisema kwamba awali alikuwa amepanga kuandaa albamu lakini sasa amebadili uamuzi ili kuendana na soko la muziki wa Kizazi Kipya lilivyo sasa.

“Kwa sasa nina nyimbo nne ambazo zinaendelea kutamba zikiwamo za "Matatizo" na "Aiyola", nitaendelea kuandaa mpya moja baada ya nyingine na kuingiza sokoni,” alisema Harmonize.


Harmonize ambaye jina lake halisi ni Rajabu Abdul alisema utaratibu wa kuandaa albamu ulikuwa na manufaa zamani lakini sasa muziki umebadilika ndiyo maana wasanii hutoa singo tu.

No comments