HARRY CANE ASEMA ANATAKA MKATABA UTAKAOMFANYA AWE MCHEZAJI GHALI EPL

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kaiweka juu timu yake ya Tottenham, staa Harry Cane amesema kuwa anataka mkataba ambao utamfanya awe mchezaji ambaye analipwa bei kubwa katika michuano ya Ligi Kuu England.


Kwa sasa Tottenham iko katika mchakato wa kumpa mkataba mpya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa klabu misimu miwili iliyopita baada ya kufunga mabao 31 katika mashindano yote msimu wa 2014/15 na uliofuata akaziona nyavu mara 28.

No comments