Habari

HISPANIA YAIFANYIA KITU MBAYA ENGLAND …dakika 2 za mwisho zabadili sura ya mchezo

on

ENGLAND imeporwa tonge kinywani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Hispania.
Kocha mpya wa England, Gareth Southgate alishuhudia timu yake ikiongoza 2-0 hadi dakika ya 88 lakini hadi mwisho wa mchezo matokeo yakawa 2-2.
Adam Lallana aliifungia England bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 9 kabla ya Jamie Vardy kupachika la pili dakika ya 48, hilo likiwa bao lake la kwanza baada ya kucheza kwa dakika 937 bila bao kwa klabu yake ya Leicester City na England.
Hispania wakachomoa bao moja dakika ya 89 kupitia kwa Iago Aspas huku Isco akisawazisha katika dakika ya za majeruhi.
ENGLAND (4-2-3-1): Hart (Heaton 45); Clyne, Stones, Cahill (Jagielka 45), Rose (Cresswell 79); Dier, Henderson; Lingard, Lallana (Walcott 27), Sterling (Townsend 65); Vardy (Rashford 67).
SPAIN (4-2-3-1): Reina; Carvajal, Martinez, Nacho, Azpilicueta; Busquets (Nolito 78), Thiago (Herrera 56); Mata (Aspas 45), Silva (Isco 64), Vitolo (Koke 45); Aduriz (Morata 64).

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *