IBRAHIMOVIC AULIZA "NANI ANASEMA MANCHESTER UNITED YA MOURINHO IMEFULIA?"

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesema wale wanaodhani kikosi cha Jose Mourinho kimefulia, lazima wajiulize mara mbili.

Msweden huyo aliyejiunga uwanja wa Old Trafford kama mchezaji huru msimu huu, amesema anachoamini yeye kwa sasa ni suala la muda tu kabla ya kikosi hicho kuchochea moto.

Ibra alimaliza ukame wa mabao baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kufunga mara mbili wakati United ikipata ushindi mara wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City kwenye uwanja wa Liberty.

“Ni suala la muda tu, mambo yatajipa,” alisema.
“Tunachosubiri hapa ni suala la muda tu mambo mengine yatakuja yenyewe ndani na nje ya uwanja.”


“Tumekuwa tukicheza vizuri na tunachokosa ni bahati kwa baadhi ya mechi,” aliongeza staa huyo.

No comments