ISCO AKANUSHA TAARIFA ZA KUTAKA KUSEPA REAL MADRID KUTIMKIA TOTTENHAM

ISCO amekanusha taarifa kuwa anataka kuhamia katika klabu ya Tottenham na kuikimbia Real Madrid.

Hatua ya Isco kuweza hadharani msimamo huo inafuatia uvumi uliopo sasa unaomtaja kutaka kuachana na kikosi hicho cha Santiago Bernabeu.

Alihusishwa na tetesi za kutaka kutua katika kikosi cha Spurs ingawa pia alihusishwa na kutaka kutua pia Stanford Bridge.
Mnamo mwezi Agosti mwaka huu alivumishwa pia kutaka kusajiliwa na Tottenham Hotspur, lakini hata hivyo dili lilishindikana.

Akikanusha, Isco alisema: “Ninahusishwa kuondoka hapa lakini ni jambo lisilo na ukweli.”

“Sio kweli kwani nina miaka miwili ya mimi kubaki hapa ndani ya Santiago Bernabeu.”

“Ingawa bado hakuna mazungumzo juu ya kandarasi yangu, lakini ninachoamini bado nitaendelea kuwepo hapa.”

“Sijajua nini kitatokea baadae lakini kuwa na msimamo ni jambo la maana na muhimu pia,” alisema Isco.


Pamoja na Tottenham pia Isco anatajwa katika uvumi wa kutua Old Trafford chini ya kocha Jose Mourinho.

No comments