JAMIE VARDY NI KAMA AMEFULIA VILE… eti msimu huu ana mabao mawili tu katika mechi 15

KWELI kafulia. Mshambuliaji Jamie Vardy msimu uliopita aliweka rekodi akiwa na Leicester City alipofunga mabao katika mechi 11 mfululizo.

Mechi 12 baadaye nyota huyo aliyekuwa mmoja kati ya wachezaji waliyoipa ubingwa wa England Leicester msimu uliopita, hajafunga bao hata moja baada ya kucheza mechi 11.

Kiwango chake bora cha kiuzifumania nyavu msimu uliopita kilimfanya kuitwa kikosi cha taifa England lakini pia alikuwa chaguo la kwanza la usajili wa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

Huwezi kutegemea kwa mchezaji aliyekuwa kinara wa mabao Leicester City msimu uliopita, msimu huu ana mabao mawili tu katika mechi 15.

Inachoshangaza zaidi ni kwamba wakati Leicester wanafanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mechi nne walizocheza, Vardy hajagusa kamba hata mara moja.


Kocha Wenger alikuwa tayari kumwaga pauni mil 20 kumtwaa Vardy uwanja wa Mfalme, lakini ni suala la muda kama kweli Wenger alikwepa mkosi au Vardy mwenyewe atajuta kukataa ofa ya kwenda Arsenal.

No comments