JB AIPIGIA TAMTHILIA YAKE YA “KIU YA KISASI”

MWIGIZAJI wa siku nyingi wa Bongomuvi, Stephen Jacob “JB” ameanza kuipigia debe Tamthilia ya “Kiu ya Kisasi” akidai kwamba hana kawaida ya kusema uongo na kuwataka mashabiki wajiandae kupata kitu chenye ubora unaotakiwa.

“Nipo katika hatua za mwisho kabisa za uhariri wa Tamthilia yetu ya “Kiu ya Kisasi” ambayo kwa asilimia 90 imekamilika, huwa sina kawaida ya kusema uongo, kazi hii ni nzuri sana inatosha kuwafanya mtoroke kazini,” alisema JB.

Alisema kuwa Tamthilia hiyo itaruka mwaka mzima kwa madai kwamba ina sehemu 50 za kusisimua na kwamba baada ya Tamthilia hiyo atatoa filamu yake ya mwisho na kisha ataachana na uigizaji.


JB ambaye pia ni mtayarishaji wa Bongomuvi alisema kuwa kwa sasa anatamba na filamu yake ya “Kalambati Lobo” na anaamini kwamba filamu ya mwisho atakayoitoa itakuwa kali.

No comments