JIMMY MASTER ASEMA YEYE NA KUNDI LAKE HAWAFANYI KAZI KWA KUKURUPUKA

KUNDI la sanaa za maigizo la Mzimuni Theatre Arts limesema halifanyi kazi kwa kukurupuka bali linazingatia umakini kusoma ishara za nyakati na kufanya kile ambacho kinakubalika kwa mashabiki.

Mkurugenzi wa kundi hilo, Jimmy Mponda “Jimmy Master” ambaye pia ni nyota wa filamu za “Action” aliyasema hayo alipokuwa akizungumzia filamu iitwayo "Foundation" iliyoandaliwa na kundi hilo.

“Umakini wa msingi sana katika uandaaji wa filamu na siyo kuandaa tu bila kuzingatia ama kusoma ishara za nyakati kwani mwisho wake ni kuandaa vitu vya ovyo vitakavyopondwa katika jamii na kisha kukwama njiani,” alisema Jimmy.


Alisema kuwa baada ya kuingiza sokoni filamu ya "Foundation" kinachofuata sasa ni kuhakikisha inapata muda wa kutosha kukaa sokoni kisha wataandaa nyingine baada ya miezi mitatu ama minne.

No comments