JOHARI AWATAKA WASANII WA KIUME BONGOMUVI KUTOWARUBUNI WASICHANA CHIPUKIZI

MKONGWE wa kike wa filamu Blandina Chagula "Johari" amewataka nyota wa kiume wa fani hiyo kuacha mchezo wa kuwarubuni wasanii wa kike kwamba watawasaidia na kisha kuwatumia bila ya msaada wowote.

Wasanii wenye tabia hiyo ndio wamekuwa wakichangia kuifanya Bongomuvi kuonekana kama ya wahuni na kumbe kuna watu wana heshima zao mbele ya jamii.

“Nina sema hivyo kwasababu ni muda mrefu sasa kumekuwepo na malalamiko kwamba wasanii nyota wa kiume wamekuwa wakiwatumia kingono chipukizi wa kike kwa ahadi za kuwasaidia kumbe mwisho wa yote hakuna lolote," alisema.

Alisema wasanii wasiojielewa hujikuta wameinga katika mtego huo na kuuza utu wao bila kupata kile ambacho huwa wameahidiwa na amewataka chipuziki kuepuka kuingia mkenge.

No comments