JOKATE ASEMA UBUNIFU WAKE KATIKA BIASHARA UMEMFIKISHA MBALI

KIMWANA mwigizaji ambaye pia anajishughulisha na mambo ya urembo Jokate Mwegelo amesema kuwa ubunifu katika biashara ndio njia pekee ambayo imemwezesha kufika pale alipo.

Licha ya kutokuwa na filamu mpya kwa muda mrefu Jokate alisema kuwa amekuwa akiishi vyema kutokana na kujishughulisha na biashara mbalimbali.


“Kwa mfano kwa sasa nimewaletea biashara yangu mpya ya mabegi ya mgongoni yenye nembo yangu ya kidoti,” alisema msanii huyo ambaye pia hujulikana kwa jila la "Kidoti."

No comments