JOKATE MWEGELO ATAMANI UANASIASA... asema nafasi ikitokea atajitosa bila woga

KIMWANA wa Bongomuvi, Jokate Mwegelo amefunguka na kusema anaweza kuwa mwanasiasa akidai kuwa alipokuwa mdogo alikuwa anapenda watu na maendeleo yao.

Alisema kuwa nafasi ikitokea atajitosa ili kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia Watanzania ingawa hakutaja nafasi ambayo anadhani anaweza kuiwania katika siasa.

Jokate alisema: “Natamani kuwa mwanasisa na kama ikitokea nafasi hiyo ninaweza kuwa mwanasiasa  kwani tangu nikiwa mdogo nilikuwa ninapenda watu na maendeleo yao."

“Kuna watu wanaona naweza kuwania uongozi na kusema ukweli kwamba ninapenda watu na maendeleo yao na ndiyo nilivyo ila inategemea kama nafasi itapatikana basi ninaweza kuwania."

No comments