JORDAN HENDERSON AIFANANISHA LIVERPOOL NA HOTELI YA NYOTA TANO

USIBISHE, Liverpool ya Jurgen Klopp inapiga soka la kitabuni acha kabisa. Nahodha wa uwanja wa Anfield, Jordan Henderson analifananisha soka la timu yake sawa na hadhi ya “hoteli ya nyota 5”.

Utalazimika kufanya kazi kubwa kuwasimamisha pacha watatu – Philippe Coutinho, Roberto Firmino na Sadio Mane.

Safu hii ya ushambuliaji ukifanya kosa dogo tu imekula kwako. Ndio maana Klopp sasa anajivuna kileleni mwa msimamo wa Ligi akikusanya mabao 30 hadi sasa.

Henderson alifurahishwa na washambuliaji hao akisema wanafanya kazi nzuri kama safu yao ya ulinzi.

“Hawa ni wachezaji wa daraja la kwanza duniani,” alisema.
“Uwezo wao wa kusoma mchezo sio tu kushambulia, lakini pia namna wanavyojituma kucheza sambamba na wenzao ni mambo ya kufurahisha.”

“Wote kwa pamoja wanawasaidia walinzi. Ni wachezaji pekee, wakiwa mbele ni vigumu kuwazuia.”

Mane, Coutinho na Fermino wameongoza safu ya ushambuliaji msimu huu Liverpool wakifunga mabao 16 pamoja Ligi Kuu England.

Henderson pia amesema anatambua mchango wa wachezaji kama Adam Lallana.


“Inafurahisha kucheza na watu kama hawa,” alisema. “Ni jukumu letu kuhakikisha tunawapa ulinzi wakati wakienda mbele kushambulia.”

No comments