JOSHUA KIMMICH AKIRI KUVUTWA NA XAVI HERNANDEZ KWENYE SOKA

KINDA wa Bayern Munich, Joshua Kimmich ametoboa siri kuwa mkongwe wa Barcelona Xavi Hernandez ndiye aliyemvutia kuwa kwenye kiwango alichonacho hivi sasa.

Kimmich mwenye umri wa miaka 21 amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha kwanza cha Bayern tangu aliposajiliwa mwaka 2015 akitokea Stuttgart.

Tangu kuanza kwa msimu huu, mkali huo ameshapasia nyavu mara saba katika michezo 12 aliyoshuka dimbani.


“Xavi ndie aliyekuwa mchezaji ninayemkubali wakati nilipokuwa mdogo,” alisema Kimmich alipokuwa akihojiwa na mtandao wa shirikisho la soka barani Ulaya “UEFA”.

No comments