JURGEN KLOPP AMSARANDIA BEKI ALEX GRIMALDO WA BENFICA

KOCHA Jurgen Klopp ni kama hajaiamini safu yake ya ulinzi, hivyo ameanza kuangalia nini cha kufanya kwa ajili ya dirisha dogo la majira ya baridi la mwezi Januari mwakani.

Katika kutambua hilo, tayari kocha huyo amewatuma mawakala nchini Ureno kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha mlinzi wa Benfica, Alex Grimaldo.

Alex Grimaldo mwenye umri wa miaka 21, ni mchezaji kijana aliyelelewa katika kikosi cha pili cha timu ya Barcelona ambaye sasa anaingizwa katika kundi la wachezaji wanaowindwa na klabu mbalimbali barani Ulaya.

Klopp ni kati ya makocha wanaovutiwa na kiwango cha beki huyo ambaye ni mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa sambamba na umakini katika kuwadhibiti washambuliaji wenye kasi.

United wameweka mzigo mezani kiasi cha pauni mil 51 kwa ajili ya kukamiloisha dili hilo mapema mwezi Januari mwakani wakiamini klabu ya Benfica hawatakuwa na kikwazo cha kumruhusu Grimaldo kutua Old Trafford.


Kwa upande wa Benfica ni kama watajitengenezea faida kwa mlinzi huyo kwani walimnunua kwa pauni mil 1.25 kutoka Barcelona, dili lililotimia mnapo mwezi Januari mwaka huu.

No comments