JURGEN KLOPP "AWAFUNDA" MASTAA WAKE KUTOHOFIA KUKAMIWA NA TIMU PINZANI

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp ni kama amewapa darasa nyota wake baada ya kusema kuwa wanatakiwa kutohofia kukamiwa timu pinzani baada wamwisho wa wiki iliyopita kukutana na Southampon.

Katika mchezo wa Jumamosi vijana hao wa Klopp walipata nafasi nyingi za kupachika mabao lakini wakajikuta wakitoka suluhu kwenye uwanja wa St Mary hivyo kujikuta wakitupwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo Mjerumani huyo halalamiki kuhusu wenye kucheza soka kupaki basi dhidi ya timu ambayo ina uwezo wa kufunga mabao ambayo wameshafunga 30 katika mechi 12 za Ligi hiyo.

“Haikuwa maana kuhofia hilo,” Klopp aliyaambia magazeti ya Uingereza.

“Unaweza kuwaagiza waje mbele na kutupa sisi nafasi ama kitu chochote,” aliongeza kocha huyo.


Alisema kuwa kabla msimu kuanza walifanyia kazi jambo hilo na ndiyo maana anasema kuwa anajisikia mwenye furaha kwa kiwango walichokionyesha dhidi ya Southampon kwa sababu wanaendelea kufanya vizuri.

No comments