JUSTIN BIEBER “ALA BATA” NA WASICHANA SITA HOTELINI

WASICHANA wawili kati ya sita waliokula “bata” na mkali wa Pop, Justin Bieber baada ya shoo yake katika ukumbi wa O2 Arena Prague, Jamhuri ya Czech wamemlalamikia msanii huyo kuwataka usiku wa manane tofauti na makubaliano yao.

Msanii huyo kabla ya kufanya shoo hiyo alitumia ukurasa wake wa facebook kuandika kwamba baada ya shoo angependa kula bata na wasichana warembo zaidi ya sita kwa muda wa saa moja.

“Baada ya shoo yangu naomba wasicha sita hadi wanane hotelini, kama kuna mrembo aliye tayari kwa hilo anitumie ujumbe mapema na malipo yote ni juu yangu, awe na tabia nzuri na ajue kuzungumza Kiingereza,”  ulisomeka hivyo ujumbe huo.


Baada ya ujumbe huo inasemekana watu wemngi waliomba kukutana na msanii huyo kwa muda huo, nae alichagua warembo sita wakakutana kula na kunywa, lakini baadae wasichana wawili wakasikika wakilalamika kwamba waliombwa kirahisi kampani zaidi usiku mnene na msanii huyo.

No comments