KINGWENDU AKIRI ALIPOTEA KUJITOSA KWENYE SIASA... asema ana safari ndefu kurudisha jina lake lililofifia

NYOTA wa filamu za vichekesho Rashid Mwinshehe "Kingwendu" amesema kuwa bado ana safari ndefu kurudisha jina lake kwenye chati akidai kwamba lilipotea baada ya kujitosa kwenye siasa.

Kingwendu alisema kuwa baada ya kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo wa Kisarawe mkoani Pwani, mwaka jana, hakuwa na muda wa kuandaa kazi mpya akiamini kwamba angeibuka na ushindi lakini bahati mbaya akakwama.

Alisema: “Tangu wakati huo mambo hayajawa mazuri hasa kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kufiwa na mama yangu mzazi lakini nina uhakika nitarudi kwenye chati tu."


“Jina langu ni kubwa sio tu kwenye filamu za vichekesho bali pia kwenye muziki hasa wa asili, kwa hiyo nitahakikisha ninaendelea kulinda hadhi yangu kwenye sanaa."

No comments