KIWANGO CHA CHIPUKIZI ZACH CLOUGH CHAITIA PRESHA TIMU YAKE YA BORTON WANDERERS

KIWANGO kilichoonyeshwa na mshambuliaji chipukizi wa Uingereza Zach Clough kimewatisha Bolton Wanderers wanaohisi anaweza kuondoka Januari mwakani.


Kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao matano katika mechi nne za hivi karibuni za Ligi daraja la Kwanza na Bolton wanaopigania kurejea Ligi Kuu wanadhani anaweza kupandiwa dau.

No comments