KIWANGO CHA DIEGO COSTA CHAMKUNA KOCHA ANTONIO CONTE

KIWANGO kinachoonyeshwa na straika Diego Costa kinaonekana kumkuna kocha wake Antonio Conte baada ya kukisifu akisema kuwa ndicho kilichowafikisha kileleni mwa Ligi Kuu England kutokana na bao alilofunga majuzi.

Majuzi Mhispania huyo alifunga bao lake la 10 katika Ligi na kuifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Middlesbrough na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa pointi moja dhidi ya Liverpool na Manchester City kwenye msimamo wa Ligi.

Kutokana na matokeo hayo Conte alijivunia jitihada zilizofanywa na mastaraika wake watatu Costa, Eden Hazard na Pedro kwa kusababisha madhara katika safu ya ulinzi ya Boro hali iliyowafanya wafanye kazi ya ziada kuwazuia hususan kipindi cha pili.

"Akiwa na mpira Diego nacheza soka tamu,” Conte aliliambia Sky Sport.


“Vilevile Eden na Pedro ni muhimu katika uwiano na wanacheza kwa kujituma ndani ya timu ni mshambuliaji wa hatari na analionyesha hilo," aliongeza kocha huyo.

No comments