KIWANGO CHA DIEGO COSTA SASA CHARUDISHA MAPENZI KWA MASHABIKI WA CHELSEA

MSIMU uliopita ilikuwa kawaida kwa mashabiki wa Chelsea kumzomea mshambuliaji wao, Diego Costa.

Kuna wakati mashabiki walitinga jukwaani na bango lenye kumponda nyota huyo wa Hispania wakimtaja kuwa “panya” aliyemsaliti Jose Mourinho wakati akifundisha Stanford Bridge.

Lakini chini ya kocha mpya, Antonio Conte, raia huyo wa Italia sio yule wa msimu uliopita. Amebadilika kupita maelezo.

Chini ya Conte, Costa anacheza rafu chache sana na kupiga mashuti mengi langoni kuliko wakati akicheza chini ya Mourinho.

Katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton, Costa alipiga mashuti yaliyolenga shabaha kwa asilimia 70.

Costa sasa anacheza vizuri, hatumii nguvu nyingi na ameingia woga wa kucheza rafu zisizo na maana kama ilivyokuwa wakati akifundishwa na Mourinho.


Na hii inaweza kuonekana kwenye orodha ya wafungaji bora hadi sasa Ligi Kuu Enfgland. Costa ndie kinara wa mabao na amefanikiwa kurejesha mapenzi kwa mashabiki ambao msimu uliopita walimuona kama msaliti na kumpa jina la “panya msaliti”.

No comments