KLABU “ISIYOJULIKANA” KUMNG’OA LIONEL MESSI BARCELONA KWA KITITA CHA PAUNI

KLABU moja ambayo haijawekwa wazi inadaiwa inamshawishi Lionel Messi asisaini mkataba mpya na Barcelona na iko tayari kumpa dau la pauni mil 85 kama fedha yake ya kuweka mfukoni kabla ya mambo ya mshahara.

Ushawishi huo umemfanya Messi ajishauri kuingia mkataba mpya wa kuchezea Barcelona ambayo amekuwa nayo tangu utotoni.

Mkataba wake na Barcelona unamalizika mwishoni mwa mwaka 2018 na Muargentina huyo bado anajishauri kuingia mkataba mpya.

Gazeti la El Mundo lilidai kuwa timu moja ambayo haikuwekwa wazi inamshawishi Messi kutosaini mkataba mpya na Barcelona na badala yake wako tayari kutoa kitita hicho kama ada yake na baadae kuingia kwenye makubaliano ya mshahara.


Ingawa gazeti hilo halikutaja klabu hiyo lakini hisia zipo kwa Manchester City ambayo kocha wake Pep Guardiola amekuwa akitamani kumsajili mchezaji huyo.

No comments