KOCHA FRANK DE BOER ADUMU CHINI YA MIEZI MITATU INTER MILAN

KOCHA Frank De Boer amedumu chini ya miezi mitatu Inter Millan baada ya juzi klabu hiyo kutangaza kumtimua.

De Boer, kocha wa zamnani wa Ajax ya Uholanzi alipewa kibarua cha kufundisha Nerazzurri Agosti 9, saa 24 baada ya mtangulizi wake Roberto Manicini kufunguliwa mlango wa kumtaka aondoke klabu hiyo ya serie A season.

“FC Internazionale Milano inatangaza kuwa leo inavunja mkataba na kocha mkuu Frank De Boer,” ilieleza taarifa ya habari ya klabu hiyo iliyotumewa kwenye tovuti juzi.

“Sasa kikosi kitanolewa na kocha wa timu ya vijana Stefano Vecchi ambaye atakaa kwenye mechi wakati wa mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Southampon,” iliongeza taarifa hiyo ya klabu.


Mancini amepigwa mechi saba kati ya 14 kikiwemo kipigo cha bao 1-0 walichopata kutoka Sampdoria Jumapili iliyopita na kuwaacha mabingwa hao wa Serie A mwaka 2010 katikja nafasi 12 kwenye msimamo wakiwa na pointi 14.

No comments